Kazi za Taasisi ya Mwalimu Nyerere
- Dar es Salaam Taasisi ya Mwalimu Nyerere 2001
- 33P.
Mwalimu Julius K. Nyerere alitumia nafasi ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere aliopozungumza na Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma tarehe 3 Agosti,1996 kutoa maelezo na ufafanuzi wa msingi kuhusu chombo hiki kipya kilichanzishwa kupewa jina lake. Mbali na kueleza sababu zilizosababisha uamuzi wa kukipa chombo hicho jina hilo, alieleza pia chimbuko la uamuzi wenyewe, madhumuni yake pamoja na upeo wa kazi zake. Yote yanajitokeza dhahiri katika utangulizi na katika majibu ya maswali aliyoulizwa na Waheshimiwa Wabunge.